Tume ya Utumishi wa Mahakama ni chombo kilicho undwa kwa mujibu wa aya ya 112 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1997. Aidha kwa mujibu wa sheria ya uendeshaji wa mahakama Na. 4/2011, Tume ya Utumishi wa mahakama mbali na kuwa na majukumu mengine, inalo jukumu la kuajiri watumishi wa kada mbalimbali wa Mahakama.
Hivyo tume ya utumishi wa mahakama inawatangazia watanzania wenye sifa zilizo ainishwa hapo chini kwa kila nafasi ya kazi na ambao wapo tayari kufanya kazi katika Ofisi za Mahakama ya Tanzania ambazo zipo katika mikoa na wilaya mbalimbali kuleta maombi yao ya kazi.
Mkaguzi wa Hesabu wa Ndani (Internal Auditor) Daraja la II TGS D - Nafasi 25
Sifa
(i) Wenye Intermediate Certificate inayo tolewa na NBAA.
(ii) Wenye shahada ya Biashara au Sanaa yenye mwelekeo wa uhasibu au Stashahada ya juu ya Uhasibu (UDA) kutoka Chuo au Taasisi yoyote inayo tambuliwa na Serikali.
(iii) Wenye Stashahada ya juu katika Uhasibu wa Serikali (Advanced diploma in Government Accounting) kutoka chuo cha uhasibu Dar es salaam (DSA)
Waombaji watapangiwa kazi Mahakama Kuu - Kanda au Ofisi ya Hakimu Mkazi Mfawidhi isipokuwa Dar es salaam. Waombaji wa nafasi hii waonyeshe Kanda/Mikoa mitatu (3) kati ya Pwani, Morogoro, Lindi, Mtwara, Ruvuma, Njombe, Iringa, Mbeya, Rukwa, Katavi, Kigoma, Tabora, Simiyu, Mara, Mwanza, Geita, Kagera, Singida, Dodoma, Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Tanga na Shinyanga ambayo wangependa kupangiwa ingawa pendekezo lao laweza lisizingatiwe.
Mwisho wa kupokea barua za maombi ni Tarehe 16/02/2015 saa 9:30 Alasiri.
Barua za maombi ziandikwe kwa mkono wa mwombaji na kuambatanisha:-
- Vivuli vya vyeti vyote vya elimu na mafunzo.
- Ufupisho wa taarifa za mwombaji (CV)
- Kivuli cha cheti cha kuzaliwa.
- Picha mbili (Passport size) zilizopigwa hivi karibuni.
Waombaji walio katika utumishi wa Umma wanapaswa kupitisha maombi yao kwa waajiri wao na walio wahi kuacha kazi katika utumishi wa Umma waeleze bayana kuwa waliacha kazi katika utumishi wa Umma.
Maombi yote yatumwe kwa njia ya Posta kwa Katibu, Tume ya Utumishi wa Mahakama ya Tanzania,
Katibu,
Tume ya Utumishi wa Mahakama,
S.L.P 8391,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA.
Home
Ajira Tanzania
Jobs in Tanzania
Jobs Tanzania
Nafasi za Kazi
Tume ya Utumishi wa Mahakama ya Tanzania
Mkaguzi wa Hesabu wa Ndani (Internal Auditor) Daraja la II TGS D - Nafasi 25
Tuesday, February 03, 2015
Mkaguzi wa Hesabu wa Ndani (Internal Auditor) Daraja la II TGS D - Nafasi 25
Related Post
- Karanga Leather Industries Company Co. Ltd (KLICL) is established as a joint venture Com
- On behalf of our client we seeks to hire a qualified candidate for the position of a Cate
- The Regional Manager – Katavi under the TANROADS Engineer consulting Unit wish to recrui
- Air Tanzania Company Limited (ATCL) is in the process of revamping its operations and has
- BRAC is one of the world’s largest development organization has extensive development pro
- Good Neighbors is an international humanitarian development NGO founded in Korea in 199