Tume ya Utumishi wa Mahakama ni chombo kilicho undwa kwa mujibu wa aya ya 112 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1997. Aidha kwa mujibu wa sheria ya uendeshaji wa mahakama Na. 4/2011, Tume ya Utumishi wa mahakama mbali na kuwa na majukumu mengine, inalo jukumu la kuajiri watumishi wa kada mbalimbali wa Mahakama.
Hivyo tume ya utumishi wa mahakama inawatangazia watanzania wenye sifa zilizo ainishwa hapo chini kwa kila nafasi ya kazi na ambao wapo tayari kufanya kazi katika Ofisi za Mahakama ya Tanzania ambazo zipo katika mikoa na wilaya mbalimbali kuleta maombi yao ya kazi.
Afisa Tawala II - TGS D - Nafasi 80
Sifa
Shahada ya kwanza kutoka Vyuo Vikuu vinavyo tambuliwa na serikali katika fani zifuatazo:-
Utawala, Elimu ya jamii, Sheria (Mwenye cheti cha Law school), Menejimenti ya Umma, Uchumi na wenye ujuzi wa kompyuta.
Waombaji watapangiwa kazi katika mahakama za Wilaya isipokuwa za mkoa wa Dar es Salaam. Waombaji wa nafasi hii waonyeshe wilaya tatu (3) zilizopo katika mojawapo ya mikoa ifuatayo:- Pwani, Morogoro, Lindi, Mtwara, Ruvuma, Njombe, Iringa, Mbeya, Rukwa, Katavi, Kigoma, Tabora, Simiyu, Mara, Mwanza, Geita, Kagera, Singida, Dodoma, Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Tanga na Shinyanga ambazo wangependa kupangiwa ingawa pendekezo lao linaweza lisizingatiwe. Aidha, baadaye watabadilishwa kazi kuwa Watendaji wa Mahakama.
Kazi za Maafisa Tawala
(i) Kuweka kumbukumbu za matukio muhimu.
(ii) Kusimamia utekelezaji wa Sheria, Sera, Kanuni na taratibu mbalimbali.
(iii) Kusimamia kazi za Utawala na Utendaji.
Mwisho wa kupokea barua za maombi ni Tarehe 16/02/2015 saa 9:30 Alasiri.
Barua za maombi ziandikwe kwa mkono wa mwombaji na kuambatanisha:-
- Vivuli vya vyeti vyote vya elimu na mafunzo.
- Ufupisho wa taarifa za mwombaji (CV)
- Kivuli cha cheti cha kuzaliwa.
- Picha mbili (Passport size) zilizopigwa hivi karibuni.
Waombaji walio katika utumishi wa Umma wanapaswa kupitisha maombi yao kwa waajiri wao na walio wahi kuacha kazi katika utumishi wa Umma waeleze bayana kuwa waliacha kazi katika utumishi wa Umma.
Maombi yote yatumwe kwa njia ya Posta kwa Katibu, Tume ya Utumishi wa Mahakama ya Tanzania,
Katibu,
Tume ya Utumishi wa Mahakama,
S.L.P 8391,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA.
Home
Ajira Tanzania
Jobs in Tanzania
Jobs Tanzania
kazi
Nafasi za Kazi
Nafasi za kazi utumishi
Tume ya Utumishi wa Mahakama ya Tanzania
Afisa Tawala II - TGS D - Nafasi 80
Tuesday, February 03, 2015
Afisa Tawala II - TGS D - Nafasi 80
Related Post
- The Regional Manager - TANROADS Njombe on behalf of the Chief Executive TANROADS is looki
- HJFMRI or locally known as “Walter Reed Program-Tanzania” is a United States of America f
- Job Position: Product Specialist CV/CRHF, Tanzania, 18000CHW Seniority level – Mid level
- Mbeya Water Supply and sanitation Authority (Mbeya WSSA) is an autonomous water supply o
- Tanzania Institute of Accountancy (TIA) is one of the Technical Institutions in Tanzania,
- The Bank of Tanzania, an equal opportunity employer and Tanzania’s central bank, is looki