Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko, Mkoani Kigoma, kupitia Kibali cha Ajira Mbadala Kumb. Na. CFC 26/205/01 ”GG”/91 cha tarehe 22 Agosti, 2017 kikisomwa pamoja na barua Kumb. Na. CFC 26/205/01 ”FF”/95 ya tarehe 12 Machi, 2018 vilivyotolewa na Katibu Mkuu – Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, anapenda kuwatangazia wananchi wote wa Tanzania wenye sifa za kuajiriwa katika Utumishi wa Umma kuleta maombi ya kazi kwa nafasi ya Mtendaji wa Kijiji III kama ifuatavyo:
Mtendaji wa Kijiji III – Nafasi 25
MAJUKUMU YA KAZI:
- Afisa Masuuli na Mtendaji wa Shughuli zote za Kijiji.
- Katibu wa Mikutano na kamati zote za Halmashauri ya Kijiji, Mtunzaji wa kumbukumbu zote za kijiji za vikao vya Kijiji pamoja na hati ya kuandkishwa Kijiji,mali za kijiji,na rejesta ya kijiji nk.
- Kuratibu na kusimamia na kuhamasisha upangaji na utekelezaji wa shughuli zote na Mipango ya maendeleo ya Kijiji.
- Kusimamia ulinzi na Utawala Bora wa wananchi (Mlinzi wa amani) katika Kijiji.
- Kusimamia utekelezaji wa sheria ndogo katika Kijiji.
- Kupanga na kuhakikisha kupitishwa kwa ratiba za vikao vya mkutano mkuu na Halmashauri ya Kijiji.
- Kuandaa taarifa mbalimbali za Halmashauri ya kijiji kwa ajili ya mkutano mkuu wa kijiji.
- Msimamizi wa mapato na kodi za kijiji.
- Mfuatiliaji wa miradi ya kijiji na kutoa taarifa kwenye halmashauri ya kijiji.
NGAZI YA MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya mshahara TGS B kwa mwezi
SIFA ZA MWOMBAJI
Wahitimu wa kidato cha nne au sita waliohitimu mafunzo ya astashahada /cheti cha mojawapo ya fani zifuatazo: Utawala, Maendeleo ya Jamii, Sheria, Uongozi na Fedha kutoka vyuo vinavyotambulika na Serikali.
Maombi yote yatumwe kupitia anwani ifuatayo :
MKURUGENZI MTENDAJI(W)
S.L.P 03,
Kakonko
MASHARTI YA JUMLA
- Mwombaji anatakiwa kutimiza masharti yafuatayo kikamilifu:,
- Awe ni Raia wa Tanzania mwenye umri usiozidi miaka 45, bila kujali jinsi, ulemavu, kabila, dini au hali.
- Aambatanishe nakala ya cheti cha kuzaliwa na Maelezo Binafsi (CV) yaliyojitosheleza kwa maana ya taarifa na mawasiliano. Pia aambatanishe picha 1 "Passport Size" iliyochukuliwa hivi karibuni na nakala za vyeti vya Taaluma (Academic) na Weledi (Professional). Transcript "Testmonials" na "Provisional Results" au Statement of Results havipokelewi.
Maombi yatakayowasilishwa baada ya tarehe na muda uliopangwa hayatafanyiwa kazi.