KUITWA KWENYE USAILI - UHAMIAJI
Kufuatia tangazo la kazi lililotolewa na Kamishna Mkuu wa Uhamiaji la tarehe 14 na 17 Februari, 2014 kwenye magazeti ya Habari Leo, Mtanzania na Daily news; kuhusu kujaza nafasi ya Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi anawatangazia waombaji kuangalia katika tovuti www.moha.go.tz na www.immigration.go.tz ambapo majina ya wanaoitwa kwenye Usaili yameorodheshwa.
Usaili utafanyika tarehe 13 Juni, 2014, katika uwanja wa Taifa.
Wasailiwa wote wafike saa moja na nusu asubuhi.
BOFYA HAPA KUPAKUA MAJINA YA WALIOITWA
Tangazo hili limetolewa na:
KATIBU MKUU
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
03/06/2014
Wednesday, June 04, 2014
KUITWA KWENYE USAILI - UHAMIAJI
✔
Chief Editor
Published Wednesday, June 04, 2014
Tags