Tuesday, August 27, 2013

Fundi wa Matengenezo ya Umeme wa Magari (Auto Electrical)

Fundi wa Matengenezo ya Umeme wa Magari(Auto Electrical)

Sifa za Mwombaji:
(a) Awe na cheti cha ufundi wa matengenezo ya umeme wa magari yaani NTA level 2 au 3 au 4. Au,
(b) Awe na Stashahada ya Ufundi wa Matengenezo ya Umeme wa Magari yaani NTA level 5 au 6.
(c) Sifa zilizotajwa kwenye namba moja hapo juu isipokuwa sifa ya kuwa na cheti cha ufundi wa magari na kuwa na leseni.

Jeshi la Polisi Tanzania katika mwaka wa fedha 2013/2014 litaajiri wahitimu wa vyuo vya Ufundi Stadi nchini na Vyuo vya Mafunzo ya Amali Zanzibar.
Wahitimu wa fani hizo wawasilishe maombi yakiambatanishwa na vivuli vya vyeti kwa Inspekta Jenerali wa Polisi, Makao Makuu ya Polisi, S. L. P. 9141, Dar es Salaam kwa kujaza fomu ya maombi iliyowekwa kwenye tovuti ya Jeshi la Polisi www.policeforce.go.tz Fomu za maombi baada ya kupokelewa, zitachambuliwa wenye sifa wataitwa kwenye usaili kwa tarehe zitakazotangazwa kwenye vyombo vya habari. Baada ya usaili majina ya waliofaulu yatatangazwa na watatakiwa kuhudhuria mafunzo ya awali katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Moshi. 

Muhimu: Mwisho wa kupokelewa kwa fomu za maombi ni tarehe 15.09.2013.
Hairuhusiwi kuwasilisha fomu ya maombi kwa mkono. Tuma kwa 
posta kupitia anuani tajwa.