Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka, anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi wazi ishirini na nne (24) kama zilivyobainishwa katika tangazo hili.
MHUDUMU WA MAKUNDI MAALUM (Nafasi 6)
SIFA ZA MWOMBAJI
Awe na Elimu ya kidato cha nne na amehitimu elimu ya cheti cha mafunzo ya miaka miwili katika fani ya maendeleo ya jamii/Ustawi wa jamii kutoka vyuo vya maendeleo ya jamii vinavyotambuliwa na serikali
MAJUKUMU YA KAZI
i i. Kutambua na kuhudumia watu walio katika makundi maalum,
ii ii. Kukusanya takwimu zinazohusu watu walio katika makundi maalum wanaopita katika vituo,
iii iii. Kutoa taarifa ya utekezaji wa kazi zake kila wiki,
iv iv. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na Elimu, uzoefu na ujuzi wake.
MSHAHARA:
Kima cha mshahara kwa nafasi zote ni shilingi 310,000/=
MASHARTI YA JUMLA
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania,
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa,
iii. Waombaji wote wawe na umri kuanzia miaka 18 hadi 45,
iv. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)watatu wa kuaminika.
v. Maombi yote yaambatane na vyeti vya kidato cha nne, taaluma, kwa wale waliohitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika waambatanishe vyeti vya mafunzo husika.
vi. Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA
vii. Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni.
viii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na Baraza la Mitihani Tanzania – (NECTA).
ix. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
Maombi yote yatumwe kwa: -
MTENDAJI MKUU,
WAKALA WA MABASI YAENDAYO HARAKA,
S.L.P 724,
DAR ES SALAAM.
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 24 Julai, 2019.
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAKUBALIWA.
Wednesday, July 17, 2019
MHUDUMU WA MAKUNDI MAALUM (Nafasi 6) - DART
Authors jobstanzania
Published Wednesday, July 17, 2019