Tuesday, October 07, 2014

Nafasi za kazi METL

Dar es Salaam, Arusha, Moshi, Tanga, Dodoma, Singida, Igunga, Manyoni, Mbeya, Kyela, Morogoro, Mwanza, Musoma, Shinyanga, Tabora, Kigoma, Bukoba, Mjombe / Makambako, Songea, Iringa / Mafinga / Ilula, Lindi / Masasi / Mtwara, and Ifakara Moja ya kampuni yetu, A-One Products and Bottlers Limited imeanzisha uzalishaji na mauzo ya bidhaa za vinywaji vya Soda - ambavyo ni Mo Cola, Portello, Mo Chungwa, Mo Embe, Mo Bomba, Mo Lemon, Mo Mint na aina mbili ya ladha Mo Malta. Tunahitaji watu wenye ujuzi na uaminifu kwa ajili ya kuendesha shughuli za mauzo kwenye matawi yetu.

Afisa - Masoka (Sales Supervisors)
Afisa masoko wote watakuwa na jukumu la kuchukua oda zote, kusimamia usambazaji wa bidhaa kwenda kwa wateja husika, na kuongeza na kupanua mauzo kwa kutumia njia za kiufasaha na kiutaalamu na ubunifu za kuwahudumia wateja awe na elimu kuanzia Diploma na uzoefu wa miaka
mitano katika mauzo ya bidhaa aina ya vinywaji katika miji mikubwa, miji midogo ,na vijiji katika eneo lake la kazi.

Wauzaji (Salemen / Salesgirls)
Kazi kubwa ni kuwahudumia wateja wote kulingana na mpangiliowa kazi na taratibu zitakazowekwa na kiongozi wake, awe anajua kusoma na kuandika anaujuzi wa miaka 2-3 katika mauzo ya bidhaa aina ya vinywaji vinavyotambulika nchini katika miji mikubwa, miji midogo na vijiji katika eneo lake la kazi.

Madereva (Drivers)
Awe ana ujuzi wa kuendesha gari na leseni hai inayomruhusu kuendesha gari na uzoefu usiopungua miaka mitatu. Awe anafahamu vizuri maeneo yote ya miji mikubwa, miji midogo na vijiji katika eneo lake la kazi
Mwombaji atatakiwa awe na wathamini wawili ambao itabidi wawe watu wanaofahamika nakupatikana iwapo Kampuni itawahitaji.

Tuma CV yako ndani ya siku 15 ya tangazo hili kupitia recruitment@metl.net au kwenye anwani iliyopo chini

National Recruitment Cell
Mohammed Enterprises (Tanzania) Limited
P.O. Box 20660,
Dar es Salaam

Contact : 0715543608, 0765580073, 0682753764