Tuesday, May 13, 2014

NAFASI ZA KAZI YA UHARIRI (MODERATOR) at JamiiForums - Nafasi 6

Jamii Media imedhamiria kuboresha kitengo chake cha uhariri wa mijadala ya mtandao wake wa JamiiForums.com ili kuweza kusimamia ubora wa mijadala anuai.

Kutokana na kuwa kitengo hiki ni kipya kwa wengi katika Jamii; sifa za ziada za muhimu zitafundishwa kwa wale watakaopata nafasi hiyo. Kitengo cha usaili kimeweka taratibu za kuhakikisha somo linatolewa kabla ya kuanza kazi ili kazi ifanywapo iwe yenye tija kwa watumiaji wa mtandao na hata wasomaji wake. Mafunzo hayo yatachukua muda wa majuma mawili kabla ya wahariri wapya kuingizwa katika utendaji.

NAFASI – UHARIRI (MODERATOR) - Nafasi 6

Atahusika katika kufuatilia na kusimamia mada kwenye Jukwaa alilopangwa. Kufuatilia na kusimamia huko kutahusisha:


  • Kufanya kazi ya uhariri kwa misingi na sheria na miongozo ya JamiiForums
  • Kusimamisha/Kurekebisha/kuhariri mada kupitia mabandiko (posts) ya mada hiyo
  • Kuwalinda washiriki wote kuwa na uhuru sawa wa kutumia Jamvi bila upendeleo wowote
  • Kuhakikisha Mada zilizopo zipo mahala panapostahili
  • Kuhakikisha mada zinazojadiliwa zinajadiliwa ndani ya hoja na washiriki na kuwa hakuna wanaoharibu hoja, kutoa matusi/kejeli/kashfa kwa washiriki na hata wasio washiriki kwa lengo la kuchakachua mada



SIFA ZA MWOMBAJI


  • Awe ni mwanachama hai (active member) wa JamiiForums aliyejiunga si chini ya mwaka mmoja (Siku ya usaili utaulizwa ID yako)
  • Awe na umri kati ya miaka 24 – 33
  • Elimu isiwe chini ya kidato cha 6
  • Awe na uwezo wa kutumia kompyuta na Mitandao mingine ya kijamii kama Twitter na Facebook
  • Awe na uwezo wa kusoma na kuandika kwa lugha ya Kiingereza na Kiswahili kwa ufasaha
  • Awe anaishi Dar es Salaam.



NAMNA YA KUTUMA MAOMBI

Tafadhali tuma Maombi yako kupitia barua pepe ya vacancies@jamiiforums.com. Barua ya maombi iambatane na CV. Ya kuzingatia katika barua ya maombi ni yafuatayo:-


  • Elezea jinsi unavyoifahamu JamiiForums (unaitazama vipi), bila kusahau unachopenda, usichopenda pamoja na ushauri wa uboreshaji kama ukipewa fursa ya kuwa mhariri (moderator)
  • Urefu wa maelezo yako usizidi maneno 1,000!



Mwisho wa kutuma maombi ni Mei 15, 2014

ZINGATIA: Nafasi hii ni ya 'Full Time' na hivyo utapaswa kufanya kazi hii ukiwa ofisi za Jamii Media - Dar es Salaam