Afisa Mifugo Msaidizi Daraja La II (Livestock Field Officer II) – Nafasi 473
Majukumu Ya Kazi
- · Atafanya uchunguzi wa magonjwa ya mifugo kwa wafugaji wa eneo lake.
- · Kwa kushirikiana na wakaguzi wa afya, atakagua nyama na usafi wa machinjio
- mara kwa mara.
- · Atakusanya takwimu za nyama na mazao yatokanayo na mifugo k.m ngozi na
- kuandika ripoti.
- · Atatibui magonjwa ya mifigo chini ya usimamizi wa Daktari wa mifugo na
- kushauri wafugaji jinsi ya kukinga mifugo dhidi ya magonjwa.
- · Atatembelea wafugaji mara Kwa mara na kuwapa ushauri fasaha wa kitaalam
- katika eneo Lake Kazi.
- · Atakusanya takwimu zote za maendeleo ya mifugo katika eneo lake .
- · Atashauri na kusimamia ujenzi wa majosho, machinjio, vibanio na miundo mbinu
- inayohusiana na ufugaji bora.
- · Atahusika na uhamilishaji (Artificail Insemination) na uzalishaji (breeding) wa
- mifugo kwa ujumla.
- · Atashauri wafugaji kuhusu mbinu bora za kuzalisha maziwa na utunzaji wa
- ndama.
- · Atafanya kazi nyingine za fani yake kama atakavyopangiwa na mkuu wake wa
- kazi.
Sifa Za Mwombaji
- · Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha VI waliofuzu mafunzo ya Stashahada (Diploma) ya mifugo kutoka chuo cha Kilimo na Mifugo (MATI au LITI) au chuo kingine chochote kinachotambuliwa na Serikali.
MSHAHARA
· Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS C kwa mwezi
Mashariti ya Jumla Kwa Kazi Zote
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania.
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za
kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iv. Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe katika kichwa cha habari cha barua na juu
ya bahasha, kutozingatiwa hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.
v. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye
anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)
watatu wa kuaminika.
vi. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya
kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya
kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho
hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka kupotea.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
vii. “Transcripts”, “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”,
hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS
SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
viii. Waombaji wawe na umri usiozidi miaka 45.
ix. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba
isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
x. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko
katika utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo
yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
xi. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za
kisheria.
xiii. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 12 Desemba, 2013
xiv. Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira
HAURUHUSIWI.
xv. Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe
kupitia posta kwa anuani ifuatayo.
Katibu, ,
Sekretariati ya Ajira katika
Utumishi wa Umma,
S.L.P 63100,
Dar es Salaam.