Afisa Uvuvi Daraja La II (Fisheries Officer Grade II) – Nafasi 39
Majukumu Ya Kazi
- · Kutekeleza Sera ya Uvuvi.
- · Uhifadhi wa samaki na viumbe wengine wa majini na mazingira yao.
- · Kuratibu na kusimamia uhifadhi wa mazingira.
- · Kuendeleza uvunaji endelevu wa samaki na viumbe wengine wa baharini,
- maziwa, mito, mabwawa na malambo.
- · Kutoa ushauri wa kitaalam kuhusu Uvuvi bora, utengenezaji na udhifadhi bora
- wa Samaki na mazao ya uvuvi, Biashara na Masoko ya Samaki pamoja na
- Ufugaji wa Samaki na viumbe wengine wa majini.
- · Kutoa leseni za uvuvi.
- · Kuendesha mafunzo ya taaluma ya uvuvi.
- · Kusimamia na kutekeleza Sheria za Uvuvi (k.m. kuzuia uvuvi haramu).
- · Kusimamia ukusanyaji wa takwimu za uvuvi pamoja na maduhuli.
- · Kuratibu shughuli za utafiti wa uvuvi.
- · Kutoa ushauri na Mafunzo kwa wananchi juu ya uendelezaji na matumizi
- endelevu ya rasilimali ya uvuvi.
- · Kukagua ubora wa Samaki na mazao ya uvuvi na kuweka viwango vya Kitaifa.
Sifa Za Mwombaji
- · Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza (Bachelor Degree) katika fani za Sayansiya Uvuvi (Fisheries Science/Management, Zoology, Microbiology, Marine Biology, Food Science and Aquaculture)
Mshahara
- · Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
Mashariti ya Jumla Kwa Kazi Zote
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania.
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za
kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iv. Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe katika kichwa cha habari cha barua na juu
ya bahasha, kutozingatiwa hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.
v. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye
anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)
watatu wa kuaminika.
vi. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya
kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya
kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho
hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka kupotea.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
vii. “Transcripts”, “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”,
hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS
SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
viii. Waombaji wawe na umri usiozidi miaka 45.
ix. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba
isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
x. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko
katika utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo
yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
xi. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za
kisheria.
xiii. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 12 Desemba, 2013
xiv. Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira
HAURUHUSIWI.
xv. Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe
kupitia posta kwa anuani ifuatayo.
Katibu, ,
Sekretariati ya Ajira katika
Utumishi wa Umma,
S.L.P 63100,
Dar es Salaam.