OUTDATED - 30 July 2012
KUITWA KWENYE USAILI
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Halmashauri ya Wilaya ya Babati, Local Government Training Institute - Hombolo (LGTI), Institute of Rural Planning Dodoma (IRDP), Cooperative Audit and Supervision Corporation (COASCO), Tanzania Official Seed Certification Institute (TOSCI), Tanzania Atomic Energy Commission (TAEC) na Taasisi ya Sanaaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) anatarajia kuendesha usaili na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi, waombaji watakaofaulu usaili.
Wasailiwa wanashauriwa kuzingatia yafuatayo:
1. Kuja na vyeti Halisi (original certificates) za kuanzia kidato cha nne, sita, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za mwombaji.
2. “Transcript”, Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
3. Kila msailiwa aje na picha moja (Passport size).
4. Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi.
5. Kila msailiwa azingatie tarehe na eneo alilopangiwa
6. Kila msailiwa aje na cheti halisi cha kuzaliwa (Original Birth Certificate)
7. Wale ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa maombi yao hayakufanikiwa na wasisite kuomba mara nafasi za kazi zitakapotangazwa tena.
Usaili utaanza saa mbili (2:00) Asubuhi na utafanyika katika mahali na tarehe kama inavyoonyesha katika nafasi husika. Wasailiwa wa taasisi kwa nafasi tajwa katika jedwali hapo chini wataanza na mtihani wa mchujo kwanza na kufuatiwa na usaili wa mahojiano kwa watakaofaulu kuendelea katika hatua hiyo.
BOFYA HAPA KWA MAELEZO ZAIDI NA MAJINA YA WALIOITWA
Monday, July 30, 2012
TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI
✔
Chief Editor
Published Monday, July 30, 2012
Tags