Friday, April 06, 2012

MHIFADHI WANYAMAPORI II – NAFASI 130

Tags

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Kumb. Na EA.7/96/01/B/40 30 Machi, 2012

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo hiki, pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma). Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi ya Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi za kazi kwa waajiri mbalimbali katika Utumishi wa Umma kama ifuatavyo:

1.0 MHIFADHI WANYAMAPORI II – NAFASI 130

Nafasi hizi ni kwa ajili ya Wizara ya Maliasili na Utalii

1.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kufanya doria ndani na nje ya maeneo ya hifadhi au mbuga za wanyama
 Kusimamia utekelezaji wa utaratibu wa uwindaji na utalii
 Kulinda binadamu na mali zake dhidi ya wanyama hatari.
 Kukusanya na kulinda nyara za Serikali
 Kufanya usafi na ulinzi
 Kubeba na kutunza vifaa vya doria
 Kudhibiti uingiaji na utokaji wa watu na mali kwenye hifadhi
 Kutunza vielelezo vya ushahidi vya nyara
 Kudhibiti wanyamapori waharibifu
 Kukagua vibali na leseni za matumizi ya wanyamapori.
Kudhibiti mioto mikali kwenye mapori.

1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kidato cha IV au Kidato cha VI
 Wenye Stashahada/Astashahada ya Uhifadhi wa Wanyamapori kutoka Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
 Waliopitia mafunzo ya nidhamu na ukakamavu yanayotolewa na vyuo vya wanyamapori watapewa kipaumbele. Wale watakaopata nafasi lakini hawana mafunzo hayo, watapewa mafunzo husika kama sehemu ya mafunzo ya “Induction”.

1.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGS.B naC kwa mwezi.

NB: MASHARITI YA KAZI .
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania.
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iv. Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe juu ya bahasha, kutozingatiwa hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.
v. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
vi. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwawale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka kupotea.

- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.

vii. Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
viii. Waombaji wawe na umri usiozidi miaka 45.
ix. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
x. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
xi. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xii. WAAJIRI WOTE WALIOPO NJE YA DAR ES SALAAM WANAOMBWA KUSAMBAZA MATANGAZO HAYA KWENYE MBAO ZA MATANGAZO NA MAENEO MENGINE.
xiii. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 13 Aprili, 2012
xiv. Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira HAURUHUSIWI.
xv. Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe kupitia posta kwa anuani ifuatayo.

Katibu,
Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma,
SLP.63100,
Dar es Salaam. 

AU
Secretary,
Public Service Recruitment Secretariat,
P.O.Box 63100
Dar es Salaam.

NB: Aidha, tangazo hili linapatikana kwenye tovoti zifuatazo: www.ajira.go.tz, www.utumishi.go.tz na www.pmoralg.go.tz