Friday, April 06, 2012

AFISA UFUGAJI NYUKI II (WAKUFUNZI) – TGS D – NAFASI 10

Tags

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Kumb. Na EA.7/96/01/B/40 30 Machi, 2012

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo hiki, pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma). Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi ya Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi za kazi kwa waajiri mbalimbali katika Utumishi wa Umma kama ifuatavyo:


3.0 AFISA UFUGAJI NYUKI II (WAKUFUNZI) – TGS D – NAFASI 10

Nafasi hizi ni kwa ajili ya Wizara ya Maliasili na Utalii

3.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kusimamia uanzishaji wa hifadhi za nyuki na manzuki.
 Kutangaza sera na Sheria za ufugaji nyuki.
 Kufundisha masomo ya fani ya ufugaji nyuki.
 Kukusanya takwimu za raslimali na ufugaji nyuki
 Kupanga na kupima ubora wa mazao ya nyuki.
 Kutayarisha mpango wa kazi (Scheme of Work) wa mafunzo.
 Kufundisha masomo ya fani husika.
 Kupima maendeleo ya Wakurufunzi katika nadharia na vitendo.
 Kutunga na kusahihisha mitihani.
 Kusimamia mitihani katika vyuo vya Maliasili.

3.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wenye Shahada katika fani ya Ufugaji Nyuki au Sayansi ya Elimu ya Mimea, Elimu ya wadudu au Elimu ya Wanyama kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na serikali.

3.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGS.D kwa mwezi.


NB: MASHARITI YA KAZI .
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania.
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iv. Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe juu ya bahasha, kutozingatiwa hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.
v. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
vi. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwawale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka kupotea.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
vii. Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
viii. Waombaji wawe na umri usiozidi miaka 45.
ix. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
x. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
xi. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xii. WAAJIRI WOTE WALIOPO NJE YA DAR ES SALAAM WANAOMBWA KUSAMBAZA MATANGAZO HAYA KWENYE MBAO ZA MATANGAZO NA MAENEO MENGINE.
xiii. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 13 Aprili, 2012
xiv. Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira HAURUHUSIWI.
xv. Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe kupitia posta kwa anuani ifuatayo.

Katibu,
Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma,
SLP.63100,
Dar es Salaam. 5

AU
Secretary,
Public Service Recruitment Secretariat,
P.O.Box 63100
Dar es Salaam.
NB: Aidha, tangazo hili linapatikana kwenye tovoti zifuatazo: www.ajira.go.tz, www.utumishi.go.tz na www.pmoralg.go.tz