Saturday, June 11, 2011

Office Assistants

Kampuni ya Maunga Tours ya mjini Moshi imefungua ofisi mjini Morogoro. Inapenda kutangaza kuwa inatafuta wasaidizi wawili watakaokuwa katika ofisi hiyo mpya

Sifa
Kidato cha nne na kuendelea
Ujuzi wa Kutumia computer (Ms Word, Internet browsing),
Umri usiozidi miaka 35

Majukumu
Kupokea watalii na orders za watalii watakaokuwa wanafanya ziara za Mbuga za Mikumi na Ruaha, na milima ya Uluguru
Kuratibu accomodations kwa watalii watakaohitaji
Kuratibu taratibu zote za safari (usafiri, chakula na afya) ya wateja
Shughuli nyingine atakazopangiwa na makao makuu Moshi, zinazihusiana moja kwa moja na shughuli za kampuni

Ilani
Atakayeajiriwa awe tayari kusafiri mara kwa mara kuwapokea na kuwatembeza watalii

Mkataba na Malipo
Kampuni itaingia mkataba wa miaka mwaka mmoja na mwajiriwa, na unaweza kuendelezwa kutokana na matakwa ya mwajiri na mwajiriwa. Maelezo zaidi yatapatikana kwenye fomu za mikataba, wakati wa interview

Malipo ya kuanzia ni Tsh 215,000/=


Kuomba
Atakayetaka kuomba awasilishe barua ya maombi kwa njia ya internet akiambatanisha na CV na nakala ya vyeti vya shule kupitia anuani; ramosaaron55@yahoo.com

Mwisho wa kupokea maombi tarehe 20/06/2011.