TANGAZO LA KAZI
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na Taasisi ya Benjamin William Mkapa HIV/AIDS inatekeleza Mradi wa kuimarisha mifumo ya huduma za afya ( Health Systems Strengthening) kupitia ufadhili wa Mfuko wa Dunia wa kupambana na UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria - Mzunguko wa 9 ( Global Fund Round 9). Baadhi ya malengo ya mradi ni pamoja na; kuongeza wataalam wa afya, ili kuimarisha huduma za UKIMWI, Kifua Kikuu, Malaria na huduma nyinginezo, katika Halmashauri zilizopo maeneo yenye uhaba mkubwa wa watumishi kutokana na changamoto ya mazingira yake.
Katika awamu ya kwanza ya mradi ( 2011- 2012), Halmashauri zilizopo katika mikoa ifuatayo zitapata watumishi wa afya wa kada mbalimbali:
Mkoa wa Mtwara: Nanyumbu, Mtwara Vijijni, Newala, Tandahimba, Masasi. | Mkoa wa Singida: Singida Vijijini, Manyoni na Iramba |
Mkoa wa Lindi: Lindi Mjini, Lindi Vijijini, Nachingwea, Ruangwa, Liwale, Kilwa. | Mkoa wa Pwani: Bagamoyo, Mafia na Kisarawe. |
Mkoa wa Rukwa: Nkasi, Mpanda/Katavi, Sumbawanga Vijijini, Sumbawanga Mjini | Mkoa wa Morogoro: Ulanga, Morogoro Vijijini, Kilosa |
Mkoa wa Ruvuma: Songea Vijijini, Namtumbo, Tunduru, Mbinga. | Mkoa wa Arusha: Monduli, Ngorongoro. |
Mkoa wa Iringa: Makete, Iringa Vijijini. | Mkoa wa Manyara: Simanjiro, Kiteto, Hanang. |
Wizara kwa kushirikiana na BMAF, inatangaza nafasi za kazi kwa wataalam wa afya 230, wa kada zifuatazo:
Taaluma | Nafasi wazi |
i. Daktari ( Medical Officer) | 14 |
ii. Mfamasia ( Pharmacist) | 5 |
iii. Katibu wa Afya ( Health Secretary) | 3 |
iv. Mteknolojia - Dawa (Pharmaceutical technician) | 4 |
v. Mteknolojia – Maabara ( Laboratory Technician) | 12 |
vi. Daktari Msaidizi ( Assistant Medical Officer) | 8 |
vii. Afisa Muuguzi Msaidizi ( Assistant Nursing Officer) | 25 |
viii. Tabibu ( Clinical Officer) | 98 |
ix. Muuguzi (Nurse) | 56 |
x. Tabibu Msaidizi ( Clinical Assistant) | 5 |
Jumla 230 |
Izingatiwe kwamba:
- Ajira ndani ya mradi huu itatolewa kwa mkataba wa miaka miwili. Kwa wale wote watakaofanikiwa kumaliza vipindi vyao vya mikataba, wataajiriwa katika utumishi wa umma.
- Watumishi waliopo katika ajira ya utumishi wa umma au katika Taasisi/Vyuo vya mashirika ya dini (FBOs) hawaruhusiwi kuomba nafasi hizi.
- Mishahara itatolewa kwa mujibu wa Waraka wa Maendeleo ya Utumishi Na. 1 wa mwaka 2009 kulingana na sifa na ujuzi wa mtumishi husika pamoja na maslahi mengineyo yaliyobainishwa katika mradi.
- Kwa taratibu za Serikali, wataalamu wenye umri chini ya miaka 45 wanashauriwa kuomba zaidi, na watakuwa na fursa kubwa ya ajira yao kuingia serikalini kwa masharti ya kudumu na pensheni. Kwa wataalamu wenye umri zaidi ya miaka 45 au waliostaafu, maombi yao pia yatashughulikiwa na ajira ya serikali itakuwa kwa mkataba.
Maombi yote yaambatanishwe na:
- Barua ya maombi ya kazi, ikipendekeza Halmashauri 3 mwombaji anayopendelea kupangwa kazi, na pia aonyesha ridhaa ya kujiunga na utumishi wa umma, baada ya mkataba wa miaka miwili kumalizika.
- Nakala ya cheti cha Taaluma na cheti cha kidato cha 4 pamoja na cha 6 (iwapo anacho), na viwe vimethibitishwa na Hakimu au Wakili.
- Picha mbili (2) – saizi ya Pasipoti na maelezo binafsi (CV), ikionyesha umri, anuani kamili na namba ya simu ya kiganjani, pamoja na anuani/ namba ya kiganjani ya wadhamini wako.
Mwisho wa kupokea maombi haya ni tarehe 15 Juni 2011
Maombi yote yatumwe kwa:
Katibu Mkuu, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, S.L.P. 9083, DAR ES SALAAM.
Tangazo hili linapatikana pia katika tovuti ya http://www.moh.go.tz