Kutana Na Mwana blogger wa week hii Ally Msangi
Hello everyone na karibuni katika mahojiano yetu ya kila week. Week hii tumepata bahati ya kufanya mahojiano yetu na mwanablogger anaye miliki blog ya Jobs Tanzania.
Karibu sana hapa na tunafurahi sana kufanya mahojiano yetu hapa na wewe. Hebu tuanze mahojiano yetu kwa kuteleza kidogo kuhusu wewe binafsi na blog yako?
Kwa jina naitwa ALLY MSANGI, Ni mwanafunzi wa mwaka wa 3 katika chuo kikuu cha SAUT (St. Augustine University of Tanzania). Nachukua shahada ya kwanza katika masomo ya Biashara (BBA). Blog yangu inajulikana kwa jina la JOBS TANZANIA BLOG ikiwa ni mahususi kwa ajili ya kutangaza nafasi mbali mbali za kazi. Na wasomaji kuweza kuzisoma nakuomba kazi hizo. Blog hii inarahisisha adha ya kuhangaika kununua magazeti kila siku na kuangalia nafasi za kazi, hivyo kwa anae taka kusoma nafasi za kazi zinazo tangazwa anapitia katika blog yangu nakuangalia ni kazi ipi ina mfaa na kuweza kutuma maombi katika anuani husika kwa urahisi zaidi
Je, wewe kazi yako ni kublog tu au hii ni kama kazi ya muda tu au hobby?
Ni hobby tu na nina jiskia furaha zaidi ninapotoa huduma hii kwa watu wanaotafuta ajira kupitia mtandao wa internet. Ila hapo mbeleni natarajia kuja kuifikisha mbele zaidi ikiwezekana kufungua RECRUITMENT AGENCY.
Nini changamoto unazozipata kwa kuwa na blog?
Changamoto ninazo zipata ni nyingi sana, ila kubwa ni uelewa wa nini maana halisi ya blog yangu, watu wamekuwa wakidhani kuwa hizo kazi ninazozi post nazitoa mimi hivyo wanajikuta wananitumia vyeti vyao, pamoja na barua za maombi ya kazi hizo n.k. wakidhani mimi ndie muajiri. Nashukuru mungu nimekuwa nikiwaelimisha na sasa kidogo wameanza kunielewa.
Ni miaka mingapi sasa umekua ukiblog?
Ni mwaka sasa tangu nianze ku blog, hapo mwanzo sikutilia maanani kwani sikuona nini faida au umuhimu wa ku blog, nilianza na blog itwayo NIPE5 BLOG na mpaka leo hii inafanya kazi. Na mwaka huu mwezi wa 05-2011 nilipata wazo lakufungua JOBSTANZANIA BLOG. Hivyo blog hii ya jobs Tanzania ina muda wa takribani miezi mitatu (3) tu.
Ni nani wasomaji wa blog yako?
Wasomaji wakuu wa blog yangu hasa ni vijana walio maliza vyuo na wana tafuta ajira, na wale wote wanao tafuta kazi kupitia mitandao internet.
Je ni mitandao gani mingine ambayo unatumia ili iweze kukusaidia kuitangaza blog yako ili iwafikie wasomaji walengwa wa blog yako? Mfano Twitter au Facebook
Nina tumia facebook kuitangaza blog yangu, unaweza kunipata kupitia facebook page na group page.
Je ni nini mkakati wako na blog yako kwa ujumla?
Mkakati wangu nikui promote blog yangu nakuifanya ifahamike zaidi Tanzania nzima
Je ni bloggers wapi ambao wewe unawaangalia na kufuata nyayo zao? Na kwanini?
Nina pendezwa sana na dada subira wa www.wavuti.com na ndie mtu nae weza kuomba ushauri na akanisaidia nakunijibu, hivyo naweza sema ndio mtu anaenipa hamasa yakuendelea kutoa huduma hii.
Ni nini baadhi ya malengo yako ya mwaka huu kwa ajili ya blogu yako au unaonaje mwenyewe kwa kipindi cha mwaka mmoja au mitano toka sasa hivi blog ya itakuaje?
Nina malengo yakuifanya blog yangu kujulikana zaidi nakuweza kufanya makampuni yaweze kutangaza nafasi zao za kazi kupitia blog yangu bila hata malipo yoyote, pili malengo yangu nikuelimisha vijana wenzangu kuhusu soko la ajira na nini kinachohitajika wanapo tuma maombi ya kazi. Kwani kwa muda huu mfupi nimegundua vijana wengi hukosa kazi kwakuwa hawajui jinsi ya kuandika hata barua za maombi ya kazi (RESUMES, COVER LETER, CV).
Natarajia pia kununua domain ya jobstanzania.com/net/org kama zitakuwa zipo wazi
Je upi ujumbe wako kwa wale watu wanaotaka kuanza kublog?
Blog ni kitu kizuri cha muhimu ni uwe na mtazamo wa nini unachotaka kukitoa kwa jamii kupitia blog yako. Watu wengi huingia katika tasnia hii ya blog kwa kuona mtu fulani ana blog na yeye anataka awe na blog bila kuwa na mtizamo wa nini atakitoa kupitia blog yake.
Asante sana kwa kufanya mahojiano haya na sisi na tunakutakia baraka tele katika masomo yako pamoja na blogs zako.
SHUKRANI ZETU
tuna ushukuru sana uongozi mzima wa TANZANIAN BLOGS AWARDS kwakutupatia nafasi hii ya mahojiano, shukrani sana kwa kuendeleza tasnia hii.